Lugha
Lugha (kar: لغة) ni utaratibu kwa ajili ya kuwasiliana kati ya binadamu au kati ya viumbe vyovyote venye akili.
Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.
Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.
Yaliyomo
Maana ya neno "lugha"
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalum na
zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
Mara chache neno lugha linatumika kwa taratibu za kuwasiliana za wanyama. Lakini taratibu hizo ni tofauti sana: Katika lugha za wanyama, sauti
moja ina maana moja tu. Lakini katika lugha za binadamu, sauti nyingi
zinaunganishwa kutengeneza maneno, na maneno mengi yanaunganishwa
kutengeneza sentensi. Hivyo mnyama ambaye anaweza kutengeneza sauti
ishirini tofauti anaweza "kusema" mambo ishirini tu. Kwa upande mwingine
mtu ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini, anaweza kusema mambo
zaidi ya millioni.
Tabia za lugha
- Lugha huzaliwa
- Lugha hukua = (kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa).
- Lugha hurithiwa
- Lugha huathiriana
- Lugha lazima ijitosheleze
- Lugha hufa
Sifa za lugha
- Lugha lazima iwe inahusu binadamu
- Sauti-sauti hufanywa na mwanadamu
- Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, c, h, d, z
- Lugha huwa na mpangilio maalumu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu ---> Silabi ---> Neno
- Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi.
Dhima za lugha
- Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari.
- Lugha hutumika kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii.
- Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii.
- Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia).
- Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila/jamii au taifa fulani.
Aina za lugha
Kimsingi lugha ni moja. Uwasilishwaji wake ndiyo huigawa katika tanzu/aina kuu mbili:- Lugha ya mazungumzo
- Lugha ya maandishi
Lugha ya mazungumzo
Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo ya mdomo - na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mazungumzo. Lugha ya mazungumzo ni kongwe, hai na halisi zaidi ya mzungumzaji na ina maana nyingi kwani mzungumzaji na msikilizaji ua ana kwa ana katika mazingira mamoja.- Stadi za lugha ya mazungumzo ni kuzungumza na kusikiliza.
Na. | Chanzo | Kikomo |
---|---|---|
1 | Kuzungumza | Kusikiliza |
2 | Mzungumzaji | Msikilizaji |
Lugha ya maandishi
Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Hii ni kiwakilisha cha lugha ya mazungumzo katika mfumo wa maandishi. Lugha ya maandishi ni changa kwani imeanza karne za hivi karibuni baada ya kuvumbuliwa kwa maandishi.- Stadi za lugha ya maandishi ni kuandika na kusoma.
Na. | Chanzo | Kikomo |
---|---|---|
1 | Kuandika/Maandishi | Kusoma |
2 | Mwandishi | Msomaji |
Nyanja za lugha
Lugha ina nyanja kuu mbili nazo ni:- Sarufi - hushughulikia kanuni za lugha
- Fasihi - hushughulikia sanaa zitokanazo na lugha husika ili kuumba kazi mbalimbali za kifasihi.
Sarufi
Kukua na kufa kwa lugha
Tangu siku za kwanza za binadamu, lugha zimekuwa zikichipuka na kukuwa na kutangaa na kufa kama kiumbe chochote mwingine. Kwa hivyo, lugha zilizokuwepo leo ulimwenguni, huenda baada ya karne nyingi kupita zikatoweka na kuzuka nyenginezo.Leo ulimwenguni mathalan, kuna lugha karibu 6,700, zikiwa 1,000 katika bara la kaskazini na kusini ya Marekani, 2,000 zikiwa kwenye bara la Afrika, 230 katika bara la Ulaya, 2,200 katika bara la Asia, na 1,300 katika bara la Oshania (Australia na nchi jirani nayo).
Kurasa zinazohusiana
- Lugha ya Kiarabu
- Lugha ya Kiesperanto
- Lugha ya Kiingereza
- Lugha ya Kiswahili
- Lugha asilia
- Lugha ya kuundwa
No comments:
Post a Comment