Friday, October 31, 2014

UHAKIKI WA kiMarx

UHAKIKI WA kiMarx

Karl Marx (1818-83) na Friedrich Engels (1820-95

  -Hawa ndio waasisi wa mtazamo huu. Hata hivyo wao wenyewe hawakuandika sana kuhusiana na fasihi.

·         Hoja tatu Muhimu

  • 1.      Katika historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake namna yake ya kufikiria; mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali. Yaani jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji mali unavyoendeshwa

2.      Mabadiliko ya kihistoria katika msingi wa uzalishaji mali yanaathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka ya jamii, na hivyo kutokeza (kwa kila wakati) tabaka tawala na tawaliwa ambayo huwamo katika mapambano na harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za kijamii. 

3.      Urazini wa mwanadamu umeundwa na itikadi, Imani, thamani ya kitu (value), na namna za kufikiri na kuhisi

·   Ni kupitia katika hivi, mwanadamu huuona ulimwengu wake, na huelezea yale yaliyomzunguka na yale anayoyaona kuwa ukweli.

ATHARI KATIKA FASIHI

Waandishi wa Ki-Marx huandika kwa kutumia falsafa ya Ki-Marx na jinsi alivyoiona historia ambapo wazo kuu ni kuwa: harakati za matabaka ndio msingi mkuu unaofanya mambo yawe kama yalivyo.

Nguvu ya Historia

Jinsi gani wanavyoweza kuufahamu ulimwengu uliopita kwa kutumia vielelezo na uthibitisho wa kihistoria.

Mfano:  Matini km. Riwaya inawakilishaje ukweli? Ukweli huo ni usahihi wa mambo ktk Jamii. Usanii ni uumbaji wa Ukweli ktk maisha?

UHALISIA WA KISOSHALISTI

Mwandishi au msanii yeyote, ajitoe kuandika na kulielimisha kuhusu tabaka la wafanyakazi. Na kwamba, fasihi ni lazima iwe ya kimaendeleo, na ioneshe mtazamo wa kimaendeleo katika jamii

Georg Lukács (1885-1971) Hungary

Nadharia yake: Kiakisiko

Kwamba mambo yote huakisi ukweli fulani wa maisha. Kazi ya fasihi huakisi mfumo fulani unaofumbuka polepole. Kutuonesha mivutano, mikizano na au migogoro iliyomo katika maisha ya jamii inayoakisiwa.

KIAKISIKO

Kilicho cha msingi ni maudhui na sio fani yake. Fani inachukua nafasi ndogo sana katika kazi ya fasihi.

Mgogoro wa Ushairi wa Kiswahili.

Brecht alipingana naye kwa kusema hatuwezi kushikilia sheria za sanaa katika muda wote kwani ukweli wa jamii hubadilika.

MKABALA WA FRANKFURT 1923-1950

Nadharia Hakiki

Theodor Adorno, Max Horkheimer na Herbert Marcuse.

 Maintained by an  ICT consultant and Director of Studies:  IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com



No comments:

Post a Comment